Tuesday, September 18, 2018

KIJANA NI NANI?   sehemu ya kwanza

          MTIZAMO ULIOPO JUU YA VIJANA.

NINI MAANA NA TAFSIRI YA KIJANA?

Kijana ni nani ?
kulingana na mtazamo wangu kijana ni mtu aliyekataliwa 
sikumoja nikiwa katika matembezi yangu niliwaona watoto wadogo wakicheza mpira wa miguu ,nikiwa bado nipo katika eneo lile niliwaona vijana waliokuwa wakihitaji kucheza pamoja na wale watoto lakini wale watoto hawakuwaruhusu wakidai kwamba wale vijana wamekomaa miguu hivyo watawaumiza
 Sikumoja pia niliwahi kumuuliza mzee mmoja 'kwanini mnapokuwa na mazungumzo huwa hamuwashirikishi vijana ?' yule mzee alidai kuwa hawezi kuruhusu vijana wachangie kwenye vikao au mazungumzo yao kwakua wao ni wahuni.
Hivyo watoto huwaona vijana kama watu wanao weza kuwadhuru wakishirikiana katika mambo yao hasa michezo.
Na wazee hawaona vijana kama kundi la wahuni.
Hii ni mitazamo ambayo ipo ndani ya watu mbalimbali yaweza kuwa sahihi kulingana na mitazamo yao ,je  kulingana na mtazamo wako wewe ni mtu wa namna gani?.

Monday, September 11, 2017

Umuhimu wa kujaribu
  Karibu msomaji wa Angelotogo blog ni matumaini yangu kua wewe ni mzima wa afya .
  Karibu tujifunze japo kwa ufupi kuhisu umuhimu wa kujaribu. 

  》》Nikiwa shule ya msingi darasa la tano nilikwenda kufanya mtihani mimi na mdogo wangu yeye alikua darasa la tatu kwa wakati ule, shule ile ilikua ya kiingereza na mimi nilikua nafahamu kiingereza kwa kiasi kidogo sana, tuliingia kufanya mtihani bila ya kujiandaa .

  》》Katika ule mtihani nilipata alama 60% na mdogo wangu alipata 100%, wakati alikua hajui kiingereza hata kidogo, nilimuuliza amefanyaje hadi akapata alama zote katika mtihani wake, Alinijibu kua amebahatisha kwakua maswali yote yalikua ya kuchagua na kujikuta anapata alama zote,

  Nilijifunza kua sio vizuri kuacha kujaribu kujibu swali la kuchagua kwa kutolifahamu hilo swali kwani ni bora ubahatishe kuliko kuacha nafasi wazi, ukijaribu unaweza kulipata hilo swali kuliko kuacha kabisa kulijibu.
》》usiogope kujaribu kufanya jambo kwa kuhofia kushindwa kulitimiza vizuri, usiogope kuanza biashara kwa kuogopa hasara, usiogope kusoma kwa kuhofia kufeli mitihani.
  》》Elimu ni kuendeleza akili yako  (education is the mind development ) Elimu sio tu kuwa na vyeti vizuri bali kua na akili iliyo endelezwa vizuri, elimu hupatikana katika mazingira yote jifunze kujifunza kutoka katika watu unaokutana nao kila siku, usiwadharau watu kwa kiwango chako cha elimu kwa kua kana elimu ambayo huwezi pia kuipata katika vyuo bora duniani kama harvard lakini utaipata kwa watu wa kawaida.
  Ni rafiki yako
Michael Angelo Togo
Barua pepe; michaeltogo99@gmail.com
(0766746918)whatsap.
  

Saturday, September 02, 2017

Always learn
We learn something from everyone who passes through our lives.. Some lessons are painful, some are painless.. but, all are priceless.

Wednesday, August 23, 2017

Importance of harmony
Welcome the leader of the Angelotogo blog, it's my hope that you are fine
  Welcome and let's share a little bit about "Harmony"
Harmony is the important thing and i can assure you that the lack of harmony is the first and often the last and only cause of failure.
   The mind of any person can adapt whatever environment but that can only happen if there is harmony.
   The system, organs, cells, nerves, and tissues they all work properly if there is harmony, if one of the any stop working, the whole system may not properly function.
  Simply harmony, means organised Energy. Harmony can make the house of the peasant to live  like the house of the king, and without harmony the king's house can live the bad life wich can't be explained easily.
Thanks for your time.
It's your friend; Michael Angelo Togo.
Email address; michaeltogo99@gmail.com

Saturday, August 19, 2017

Tatizo sio kwamba tunatumia 10% ya ubongo

Habari za asubuhi mpendwa msomaji wa Angelotogo blog
Ni matumaini yangu wewe ni mzima wa afya ,karibu tujifunze kutoka kwenye makala yetu

Tatizo sio kwamba tunatumia asilimia 10 ya ubongo, tatizo ni kutokujua kuutumia ubongo.

Wanasayansi wanadai kua binadamu wengi hutumia asilimia kumi tu ya ubongo wao, watu wengi wanatamani japo ingewezekana wakatumia asilimia 100% ya ubongo wao,
 
  Japo wengine hawajatambua bado namna ya kutumia asilimia hizo 10 % .

Ubongo ndio umebeba kitu kinachoitwa na wengi akili,

   》》Akili ya binadamu ni kama betri ya simu anbayo kuna wakati inapungukiwa chaji, kama kawaida ya betri inapo ishiwa chaji lazima uichaji tena, Akili yako kuna wakati inapungua kama ilivyo kwa betri ambapo lazima uichaji.

  》》Je nitaichaji vipi akili yangu endapo itapungua, ?
Kwa kawaida kama betri inatumika lazima itaishiwa chaji, akili yako huchajiwa na vitu inavyo vipokea, kwakua akili yako nikama kituo cha kupokea taarifa na kutoa taarifa  (receiving and broadcasting centre ).

   》》 Akili yako huchajiwa kwa kusoma, kusikiliza vitu muhimu kutoka katika sehemu mbalimbali ,mtu anaye soma gazeti, vitabu, makala, nukuu, anaichaji akili yake
Ndio maana kuna utofauti mkubwa kati ya mtu ambaye hasomi hata gazeti na mtu anaye soma gazeti hata la udaku tu,

   》》Jitahidi kutumia asilimia 10%  vizuri, kwakua binadamu hatuachi kusoma hadi tunapofariki na kuna elimu ambayo pia huwezi kuipata chuo cha  harvard, jifunze kadri uwezavyo .

Ahsante ni rafiki yako
Michael Angelo Togo
Barua pepe; michaeltogo99@gmail.com.
0766746918 (whatsap).

Monday, August 14, 2017

Wednesday, August 09, 2017

Mbona hujachimba dhahabu iliyopo kwenye himaya yako
Karibu msomaji wa Angelotogo blog,
Ni matumaini yangu umeamka salama.
Nianze na swali, Je ungetambua kuwa kuna dhahabu ambayo ipo katika ardhi yako ,jambo zuri ipo kina  kifupi kama mita 2 , ungechukua jukumu gani?
Ni dhahiri ungeanza kuandaa mikakati na ungeanza uchimbaji mapema ili ujiimalishe kiuchumi,
Dhahabu inayopatikana mahara ulipo ni kila fursa iliyopo katika mazingira yako, kumbuka kila binadamu anakabiliwa na changamoto mbalimbali, "mwandishi na mhamasishaji mmoja, Edius katamgora; aliwahi kuandika katika makala yake kua ""kuna mtu anahitaji umtatulie matatizo ili akulipe fedha nzuri "
>>watu hununua ubinadamu wako na sio bidhaa, je umewahi kujiuliza kwanini kuna watu wanao fanya biashara ya aina moja lakini mmoja kati yao anakua na mauzo mazuri mwingine anapata mauzo hafifu.
  
  >> Unavyo wajali watu na kuwasikiliza na kuwashauri vizuri ndio vitu vitakavyo wavutia wateja waje kwako .
  >>Biashara ya jumla ina changamoto kubwa moja ,huwa inahitaji mtaji mkubwa,
    >>Biashara ya rejareja ina changamoto kubwa moja, inahitaji( site ) eneo zuri lililo changamka ambapo watu wanapita kwa wingi.
   Biashara ya jumla inafanyika eneo lolote, lakini rejareja inahitaji site nzuri ,ndio utapata mafanikio katika biashara yako
Ni rafiki yako na mhamasishaji
Michael Angelo Togo.
michaeltogo99@gmail.com
+255766746918 (whatsap)
Ahsante

Tuesday, August 08, 2017

Friday, July 21, 2017

Taaluma zinazoweza kukuwezesha kuajiriwa popote na kupata mshahara mnono
Tunatumia muda mwingi sana kusoma taaluma tunazozipenda katika vyuo mbalimbali nchini na nje ya nchi .

  >>Hakuna mtu yeyote katika soko la ajira asiye tamani mshahara mnono, kiwango cha kazi huenda sambamba na ngazi ya elimu uliyonayo ,mtu hawezi kusoma kwa miaka mitano mwingine mitatu alafu wakalingana mshahara .

  >>Kila mtu hulipwa kulingana na mahitaji ya taaluma hiyo kwenye ajira na kuhitaji watu wenye ujuzi katika fani hiyo na wanao jitoa katika kazi.
  Kutokana na sababu ikiwemo kukosa elimu juu ya kuchagua nini cha kusoma watu wengine husoma kozi zenye mishahara midogo sana.
   Kwa sana hizi ni baadhi ya taaluma zenye mishahara mikubwa duniani, japo kiwango chaweza kubadilika kulingana na nchi husika.

   1; SHERIA .
Wanasheria hutumia akili sana katika kufanya kazi zao, hivyo hupata fursa nyingi katika sekta binafsi na serikalini. Wanasheria hufundishwa kutoa ushauri wa kisheria kwa wateja wao /wahalifu, hii taaluma huchukua miaka mitano hadi saba inategemea na nchi, lakini mwanasheria anayekidhi vigezo hulipwa Kwa wastani dola za kimarekani 133,260 kwamwaka.

   2;RUBANI.
Kuwa rubani kunahitaji mahitaji maalumu kadhaa kama, shahada ya masuala ya anga, masaa mengi ya kujifunza kwa vitendo na huchukua miaka hadi saba katika masomo, Rubani mwenye vigezo vya kutosha hupokea takribani dola za kimarekani 140,260 kwa mwaka. 

3;UPASUAJI  (SURGEON ).
Taaluma hii ni ya watu walio bobea katika kazi ya upasuaji wa aina mbalimbali kama njia ya matibabu Kwa magonjwa ,mishahara yao huwa minene, kuna upasuaji wa aina mbalimbali kama wa mifupa, neva,
Daktari bigwa wa upasuaji hupata mshahara wa dola za kimarekani 240,440. kwa mwaka.

4;DAKTARI WA MAGONJWA YA  WANAWAKE  (GYNEOLOGIST).
Madaktari hawa hutoa matibabu katika sehemu za mfumo wa uzazi, kama vile kujifungua, ujauzito, afya ya uzazi na njia ya mkojo.
Maranyingi Daktari huyu hutumika kama mshauri kwa Madaktari wengine, huweza kufanya pia kazi kliniki,hospitali au mwalimu wa chuo kikuu, hupokea mshahara wa dola za kimarekani 214,750.kwa mwaka 

5;DAKTARI WA MENO /KINYWA  (ORTHODONTIST ).
Wataalamu walio somea hii fani huitwa orthodontist.
Wataalamu hawa hupata elimu ya kugundua tatizo, kurekebisha,meno yeyote.
Matibabu hutegemea tatizo lakini matibabu ya jumla hujumuisha kuunga au kuziba meno yaliyotoboka ,kung'olewa na matatizo mengine, taaluma hii hutoa mshahara wa dola za kimarekani 221,000.kwa mwaka. 

Tafadhali chagua vizuri nini cha kusoma
Ahsante sana
Mshirikishe na rafiki yako.