Karibu msomaji wa Angelotogo blog ni matumaini yangu kua wewe ni mzima wa afya .
Karibu tujifunze japo kwa ufupi kuhisu umuhimu wa kujaribu.
》》Nikiwa shule ya msingi darasa la tano nilikwenda kufanya mtihani mimi na mdogo wangu yeye alikua darasa la tatu kwa wakati ule, shule ile ilikua ya kiingereza na mimi nilikua nafahamu kiingereza kwa kiasi kidogo sana, tuliingia kufanya mtihani bila ya kujiandaa .
》》Katika ule mtihani nilipata alama 60% na mdogo wangu alipata 100%, wakati alikua hajui kiingereza hata kidogo, nilimuuliza amefanyaje hadi akapata alama zote katika mtihani wake, Alinijibu kua amebahatisha kwakua maswali yote yalikua ya kuchagua na kujikuta anapata alama zote,
Nilijifunza kua sio vizuri kuacha kujaribu kujibu swali la kuchagua kwa kutolifahamu hilo swali kwani ni bora ubahatishe kuliko kuacha nafasi wazi, ukijaribu unaweza kulipata hilo swali kuliko kuacha kabisa kulijibu.
》》usiogope kujaribu kufanya jambo kwa kuhofia kushindwa kulitimiza vizuri, usiogope kuanza biashara kwa kuogopa hasara, usiogope kusoma kwa kuhofia kufeli mitihani.
》》Elimu ni kuendeleza akili yako (education is the mind development ) Elimu sio tu kuwa na vyeti vizuri bali kua na akili iliyo endelezwa vizuri, elimu hupatikana katika mazingira yote jifunze kujifunza kutoka katika watu unaokutana nao kila siku, usiwadharau watu kwa kiwango chako cha elimu kwa kua kana elimu ambayo huwezi pia kuipata katika vyuo bora duniani kama harvard lakini utaipata kwa watu wa kawaida.
Ni rafiki yako
Michael Angelo Togo
Barua pepe; michaeltogo99@gmail.com
(0766746918)whatsap.
Michael Angelo Togo
Barua pepe; michaeltogo99@gmail.com
(0766746918)whatsap.
0 maoni: