"Fanya ndoto zako ziishi, ili Kupata kitu fulani, unapaswa kua na imani, kujiamini,na kufanya kazi kwa juhudi"
Katika kipindi chote cha maisha yangu mara kwa mara nimekua nikiwa na ndoto mbalimbali ninazo tamani kuzitimiza, lakini kuna zingine nimefanikiwa kuzitimiza kwa kiasi fulani na kushindwa kutimiza zingine. Ili kutimiza ndoto zako kuna hatua muhimu unazopaswa kuzipitia.
1#Chagua ndoto moja muhimu ya kutimiza .
Watu wengi wana ndoto nyingi kiasi cha kushindwa wapi pa kuanzia na wengine hushindwa kabisa kutimiza hata moja wapo ,waweza kua na ndoto ya kua muandishi wa vitabu,kumiliki nyumba, mwanzo wa kuanza kutimiza ndoto zako ni kuanza kwa kuchagua ndoto unayopenda kuitimiza na kuweka mikakati ya kuitimiza .
2#Amini ndoto yako itatimia .
Watu wengi hushindwa kutimiza ndoto zao kwa sababu ya kushindwa kujiamini na kujikubali kua wanaweza "jikubali kwanza ndio wengine wakukubali kwani usipo jikubali utawaona wanafiki"kuna watu wengine tangu wamezaliwa huwa hawajiamini, hivyo kama upo Katika hili kundi unapaswa kuwa na juhudi za kuondokana na hali ya kutokujiamini nashauri usome makala mbalimbali yanayoelezea namna ya kuongeza kujiamini, Ni muhimu pia kama unajiamini uhamishie kujiamini kwako Katika kutimiza ndoto zako.
3#Omba msaada .
Kuna watu wengi wamekutangulia na wanao uzoefu katika mambo mbalimbali, jitahidi kujifunza zaidi kadri utavyoweza, kila kitu usicho kifahamu kuna mtu anakifahamu vizuri jambo la muhimu ni kua msikivu na mvumilivu ili upate msaada.
4#Badili mfumo wa maisha yako.
Kama bado hujatimiza ndoto zako ni vizuri ukaacha kuishi kwa mazoea na kusubiri mambo yatokee yenyewe ,andaa mikakati ambayo unaamini itakusaidia kutimiza ndoto zako.
5#Jipangie muda utakao utumia ili uweze kutimiza ndoto zako.
Ndoto ambazo hazijawekewa muda wa kuzitimiza huwa ni matamanio, ukijipangia muda itakubidi uwajibike ipasavyo ili utimize ndani ya muda, kwa mfano unaweza kupanga kukamilisha ujenzi wa nyumba yako ndani ya miaka mitano ,hii ndio mipango.
6#Shirikisha marafiki kuhusu ndoto zako.
Hadi sasa watu ambao nilisha washirikisha kuhusu ndoto zangu walinitia moyo sana, na kila wakati hunitia moyo hivyo nimejikuta nikiona kama nina deni kwakua wanapenda nitimize ndoto zangu hivyo nikishindwa ntakua nime waangusha sana na gharama ya kuwaangusha marafiki zangu nikubwa hivyo nakua na ari ya kujituma ili nisiwaangushe.
7#Kuwa mvumilivu.
Kwenye harakati za kutimiza ndoto zako lazima upitie changamoto za kushindwa, lakini wenye uvumilivu ndio watakao yafikia mafanikio ya kuitimiza ndoto zao, kwa upande mwingine wale ambao hawataweza kuhimili changamoto na wakakata tamaa watarudi hadi hatua ya kwanza 1# lakini umeshafika hatua ya karibu ili kutimiza ndoto zako kwanini urudi hadi hatua ya 1#
Ni rafiki yako;Michael Angelo Togo
Barua pepe;michaeltogo99@gmail.com
0766746918 (whatsap).
0 maoni: