MTIZAMO ULIOPO JUU YA VIJANA.
NINI MAANA NA TAFSIRI YA KIJANA?
Kijana ni nani ?
kulingana na mtazamo wangu kijana ni mtu aliyekataliwa
sikumoja nikiwa katika matembezi yangu niliwaona watoto wadogo wakicheza mpira wa miguu ,nikiwa bado nipo katika eneo lile niliwaona vijana waliokuwa wakihitaji kucheza pamoja na wale watoto lakini wale watoto hawakuwaruhusu wakidai kwamba wale vijana wamekomaa miguu hivyo watawaumiza
Sikumoja pia niliwahi kumuuliza mzee mmoja 'kwanini mnapokuwa na mazungumzo huwa hamuwashirikishi vijana ?' yule mzee alidai kuwa hawezi kuruhusu vijana wachangie kwenye vikao au mazungumzo yao kwakua wao ni wahuni.
Hivyo watoto huwaona vijana kama watu wanao weza kuwadhuru wakishirikiana katika mambo yao hasa michezo.
Na wazee hawaona vijana kama kundi la wahuni.
Hii ni mitazamo ambayo ipo ndani ya watu mbalimbali yaweza kuwa sahihi kulingana na mitazamo yao ,je kulingana na mtazamo wako wewe ni mtu wa namna gani?.
0 maoni: