Thursday, July 13, 2017

Usijilinganishe na wenzako

Karibu msomaji wa angelotogo blog, 
   Ni matumaini yangu wewe ni mzima na unaendelea na jitihada za kutafuta maisha bora.
>>kwa nini usijilinganishe na wenzako?
Duniani kila mtu anamipango yake na malengo tofauti tofauti, kuna watu wana malengo makubwa, na wengine wana malengo madogo
 
   >>>Kila mtu hujipangia mikakati binafsi kulingana na malengo yake, nikiwa shule ya msingi nilikua na rafiki yangu siku zote alitamani kuwa wa kwanza darasani na ndivyo ilivyokua ,lakini ilitokea siku moja akashika nafasi ya pili darasani ,nilimshuhudia akiwa analia kwa sababu hakushika nafasi yakwanza, mimi nilikua namba ya mbali kidogo lakini nilikua nafuraha kwakua mpango wangu ilikua niwe miongoni mwa watu kumi bora darasani na mpango wangu ulitimia ndio maana nilikua mwenye furaha.

   >>Kuna watu wengine wana malengo yakua walimu wa shule za awali hivyo haitaji kuumiza kichwa sana, lakini ndugu yangu ukimuiga au ukijaribu kujilinganisha na mtu kama huyu na ukiwa na mipango mikubwa labda hata unapanga kua  rubani ,huwezi kufikia malengo yako kwakua ili uwe rubani inabidi uweke mikakati kwani kila mpango una mikakati yake itakubidi muda wako mwingi uutumie kusoma kwa juhudi na maarifa ya hali ya juu.

  
   >>Ishi kulingana na mipango yako, usiige mtindo wa maisha ya mtu fulani, anaweza kukufanya usifikie malengo yako.
Ahsante sana
Ni rafiki yako; Michael Angelo Togo
Barua pepe; michaeltogo99@gmail.com
Maoni yako ni muhimu

0 maoni: