Saturday, August 19, 2017

Tatizo sio kwamba tunatumia 10% ya ubongo

Habari za asubuhi mpendwa msomaji wa Angelotogo blog
Ni matumaini yangu wewe ni mzima wa afya ,karibu tujifunze kutoka kwenye makala yetu

Tatizo sio kwamba tunatumia asilimia 10 ya ubongo, tatizo ni kutokujua kuutumia ubongo.

Wanasayansi wanadai kua binadamu wengi hutumia asilimia kumi tu ya ubongo wao, watu wengi wanatamani japo ingewezekana wakatumia asilimia 100% ya ubongo wao,
 
  Japo wengine hawajatambua bado namna ya kutumia asilimia hizo 10 % .

Ubongo ndio umebeba kitu kinachoitwa na wengi akili,

   》》Akili ya binadamu ni kama betri ya simu anbayo kuna wakati inapungukiwa chaji, kama kawaida ya betri inapo ishiwa chaji lazima uichaji tena, Akili yako kuna wakati inapungua kama ilivyo kwa betri ambapo lazima uichaji.

  》》Je nitaichaji vipi akili yangu endapo itapungua, ?
Kwa kawaida kama betri inatumika lazima itaishiwa chaji, akili yako huchajiwa na vitu inavyo vipokea, kwakua akili yako nikama kituo cha kupokea taarifa na kutoa taarifa  (receiving and broadcasting centre ).

   》》 Akili yako huchajiwa kwa kusoma, kusikiliza vitu muhimu kutoka katika sehemu mbalimbali ,mtu anaye soma gazeti, vitabu, makala, nukuu, anaichaji akili yake
Ndio maana kuna utofauti mkubwa kati ya mtu ambaye hasomi hata gazeti na mtu anaye soma gazeti hata la udaku tu,

   》》Jitahidi kutumia asilimia 10%  vizuri, kwakua binadamu hatuachi kusoma hadi tunapofariki na kuna elimu ambayo pia huwezi kuipata chuo cha  harvard, jifunze kadri uwezavyo .

Ahsante ni rafiki yako
Michael Angelo Togo
Barua pepe; michaeltogo99@gmail.com.
0766746918 (whatsap).

0 maoni: