Kuanzisha chaneli ya YouTube ni njia rahisi ya kujipatia fedha kupitia intaneti na haihitaji uwekezaji wowote
YouTube inapata karibia video bilioni tano zinazo tazamwa kila siku na hii inadhihirisha uwezo wa kipekee ilio nao katika intaneti
FElix KJELLBERG Aambaye ni mmiliki wa chaneli ya YouTube iitwayo PewDiePie
Mwaka 2015 alijipatia kipato cha shilingi dola milioni kumi na mbili kupitia chaneli yake ya YouTube
Nawewe pia unaweza kujipatia mafanikio kama haya ukitumia vizuri fursa hii kutoka YouTube
Hii itakufaa zaidi kama :;
Unapenda kutengeneza video zako kwa kutumia simu yako au kamera ya kurekodi ,yaweza kua kwa kutoa maada fulani au kuaandaa vipande vidogo vya filamu .
Kigezo kinacho hitajika;
Kua na uwezo wa kutengeneza video fupi kwa kutumia simu yako au kamera ya kurekodi.
Muda utakao utumia hadi uweze kutengeneza chaneli yako ;
Unaweza kuanzisha chaneli yako ndani ya dakika moja tu, na punde baada ya kutengeneza utaanza kuweka video zako (upload )
MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA.
1;Tengeneza chaneli anbayo itakua mahususi kwa kitu fulani, michezo, vituko, ushauri kuhusu mambo mbalimbali n.k
2;Chagua kitu unacho kipenda zaidi ndio ukianzishie chaneli YouTube ,kwani ukifanya jambo unalo lipenda utajitoa kikamilifu.
3;Kadri utakavyokua ukipata watazamaji wengi ndio utazidi kunufaika zaidi hivyo jitahidi kuweka video katika chaneli yako zitakazo wavutia watu wazitazame kwa wingi.
4;Jitoe kikamilifu kusikiliza maoni yanayo andikwa katika chaneli yako, yasome kwa makini,itakuimalisha zaidi.
5;Peleleza kuhusu ushindani uliopo na jaribu kujifunza kuhusu vitu vinavyo wafanya wawe na mafanikio zaidi yako, epuka kunakili video zao, jitahidi kuwa wa tofauti *(uniqueness ).
6;Jitahidi kuboresha kila video unayo weka kwenye chaneli yako jitahidi iwe bora zaidi ya ile uliyo iweka mwanzo.
7;Mwisho jitahidi kushirikiana na wenzako ambao wanamiliki chaneli yenye maudhui kama yako, jifunze mbinu mpya na hii itafanya maajabu katika chaneli yako.
Namna ya kupata pesa,
Kanuni inayotumika katika ni nyepesi sana, IDADI YA WATAZAMAJI WA VIDEO KATIKA CHANELI YAKO =KIASI CHA FEDHA UTACHOLIPWA NA YOUTUBE.
Nikutakie kila la kheri unapo jaribu kujikwamua.
Ni rafiki yako MICHAEL ANGELO TOGO.
Barua pepe;michaeltogo99@gmail.com
(0766746918)
Usisahau ku *follow by email upate makala moja kwa moja katika barua pepe yako
Ahsante
0 maoni: