Sunday, June 18, 2017

Namna ya kufanikiwa katika maisha

Karibu msomaji wa angelotogo blog.


Maisha 
Kila mtu anao mtazamo tofauti kuhusu ni namna gani watakayo itumia waweze kufanikiwa katika maisha, kila mtu anao uzoefu mbalimbali kutokana na changamoto ambazo tumewahi kuzipitia, mtu aliye fanikiwa katika maisha, haina maana kwamba hajapitia changamoto ngumu ,lakini ni wabunifu, wepesi kubadilika ili kukabiliana na changamoto hizo, pia wanajituma na kujiamini .

Hatua nne kuelekea kwenye mafanikio.
 1;Orodhesha mambo yote unayo tamani uyafanikishe katika maisha yako
 Fikiria kwa kina kisha andika mambo yote unayo tamani ufanikiwe, ni vyema uyaandike kwenye 'diary 'yako ,chunguza pia tabia zako kama vile uhusiano ulionao na marafiki zako na familia yako pia.

2;Orodhesha njia utakazo zitumia uweze kuyafikia malengo yako
Orodhesha njia zote na kisha uchague njia ambazo unadhani zitakufaa zaidi ,usichague njia ambazo unauhakika hazitakupatia matokeo chanya ,ukichagua njia amini itakua sahihi, kwakua hamna kitu chenye nguvu kama imani anayokua nayo mtu.

 3;Orodhesha malengo yako yote, ukianza na lengo kuu.
Orodhesha malengo ya muda mfupi, mipango ya muda mrefu, mipango utakayo jiwekea ndio itakayokua dira yako ya mafanikio, jiwekee dira nzuri ili usije ukapotea, kua mtafiti na mwenye kujituma ili ndoto yako itimie, kama una lengo la kuwa mkulima, mjasiria mali, au msanii chagua lengo kuu na uwekeze nguvu njingi katika lengo kuu, kwakua ndio unalo lipenda zaidi, kumbuka ukifanya jambo unalo lipenda kwa dhati hata kama ni gumu sana, huonekana jepesi kwako.

4;Mfano wa kuigwa .
Kua na mfano wa kuiga ni jambo muhimu sana, japo ni vizuri mtu unae mchagua ili awe mfano wako wa kuigwa ,lazima awe na uwezo, na anajituma
Anaweza akawa msanii, mwanariadha, au mtu yeyote unae tamani kuwa kama yeye na siri moja ya kufanikiwa iliyofichika kama una mfano wa kuiga "NI KUAMINI UNAWEZA KUWA BORA ZAIDI YA MFANO WAKO WA KUIGWA "

AHSANTE SANA

Ni rafiki yako; MICHAEL ANGELO TOGO.
Barua pepe; michaeltogo99@gmail.com

Maoni yako ni muhimu ili kuendelea kuboresha kila makala .

0 maoni: