Mafanikio yamegawanyika katika nyanja mbalimbali na yapo katika namna mbalimbali, nikiwa namaanisha kwamba kila mtu ana malengo yake kulingana na anacho tamani kukifanikisha katika maisha yake
Kwa mwanafunzi mafanikio ni kufaulu mitihani kwa kiwango kikubwa
Kwa mwanariadha mafanikio ni Kutwaa medali katika mashindano
Kwa madaktari mafanikio ni kufanikiwa kuokoa maisha ya wagonjwa
Kwa lugha rahisi mafanikio yanatofautiana kulingana na mahitaji na mipango ya mtu fulani
Watu wanaelezeaje maana ya mafanikio ?
"Mwanzo wa mafanikio yoyote ni matamanio, weka hili jambo kichwani mwako wakati wote ,matamanio dhaifu huleta matokeo dhaifu, kama ilivyo kwa moto ukiwa mdogo huleta joto dogo " NAPOLEON HILL
"mafanikio ni hali ya akili, kama unataka kufanikiwa, anza kufikiri juu yako kuhusu mafanikio " MIKE DITK
Lakini ukimuuliza mtu yeyote ambaye hajafanikiwa kuhusu mafanikio ,huelezea mafanikio kua "MAFANIKIO NI SWALA LA BAHATI"
0 maoni: