Friday, June 23, 2017

Kwa nini umekata tamaa ?

 Unajua kwa nini umekata tamaa? 
 "UKIJIPANGIA MALENGO MAKUBWA, ANGALIA YASIWE JUU YA UWEZO WAKO "

 Idadi kubwa ya watu huhitaji kutimiza malengo makubwa katika kipindi kifupi, unapo jipangia malengo makubwa sana ,na muda wa kuyatimiza ukawa mfupi, ni rahisi kushindwa kuyatimiza, na mara nyingine husababisha ukate tamaa sana.

  Hakuna tatizo endapo umeamua kujipangia malengo makubwa sana, lakini kwa upande mwingine ukiwa na malengo makubwa sana ambayo endapo utashindwa kuyatimiza ,itakufanya uwe mtu wa kukata tamaa

 Ukiwa  na malengo ambayo unaweza kuyamudu itakufanya uwajibike kwa ufasaha, tatizo hutokea endapo haujajitambua kuhusu uwezo wako na njia utakazo zitumia ili uweze kuyakalibia malengo yako kwa karibu zaidi kila siku. 

  Haina maana kujiwekea malengo ambayo hujayawekea mikakati yoyote .

Japo ni sifa yetu binadamu kuhitaji mafanikio kwa haraka, lakini ni vyema ukachagua jambo angalau moja ambalo unaamini utaweza kulifanikisha kwa usahihi wake. 

Ni rafiki yako; Michael Angelo Togo 
Barua pepe; michaeltogo99@gmail.com


See you at the top www.angelotogo.blogspot.com

0 maoni: