Karibu msomaji wa Angelotogo blog ni matumaini yangu uko salama
Inaumiza sana ambapo ndugu na rafiki zetu hutoa ushauri usiokua na manufaa yoyote
Hapa nimekuwekea kauli 9 mbaya zaidi zisizofaa kusikika masikioni mwa mtu mwenye msongo wa mawazo
1:"kuna watu wana matatizo zaidi yako na hilo unalitambua "
Kauli hii haisaidii kwa namna yoyote ile, mtu mwenye msongo wa mawazo anahitaji mtu wa kukaa nae karibu na epuka kutoa kila neno linalokuja kichani kwako, unaweza kumfariji kwa kuhakikisha unakua nae karibu katika kipindi chote
2:"Maisha ni magumu "
Hii kauli humuumiza na kumfanya ahisi duniani sio mahali sahihi pa kuishi, unaweza kujaribu kua nae na kumpatia msaada hadi atakapoondokana na ile hali
3:"kabiriana na hiyo hali "
Kauli hii hufikisha ujumbe mbaya ambapo mtu hujihisi kua mpweka na kutengwa na rafiki zake wa karibu, njia nzuri yawezakua kumpigia simu na kumtumia ujumbe mfupi wa faraja .
4:"Maisha yataendelea tu"
Kuishi na msongo wa mawazo ni sawa na kuishi ukiwa umebeba mzigo mzito sana kichwani, kwa kua unapokua na mzigo mzito kichwani utatamani kusimama na utembee lakini hutoweza ,kauli hii huonyesha kua hauhusiki kwa namna yoyote na matatizo ya rafiki yako.
5:"Nenda sehemu za starehe ukapunguze mawazo "
Kutoa kauli hii kwaza ina maana hauhusiki na matatizo ya rafiki yako, ukiatoa hili wazo basi uwe tayari kwenda na rafiki yako na umpe ushauri na mawazo mapya waweza kumpigia simu na kumshauri nini afanye.
6:"maumivu na msongo wa mawazo ni kitu cha kawaida "
7:"Wewe ni jasiri utakua sawa "
Ni kweli kuna watu wana ujasiri wa hali ya juu na yamkini wamesha pitia changamoto nyingi ,bali mtu anavyokua na msongo wa mawazo anaona haina maana ya kuishi hivyo ni vizuri kua karibu
na rafiki yako.
8"Unapaswa kupambana zaidi "
Kutoa kauli ngumu kama hii kwakua inamkumbusha mtu maumivu, namna alivyo pambana lakini hakupata alicho kitegemea pia inaonyesha kujitenga kwamba matatizo ya rafiki yako hayakuhusu .
9:"Jifunze kuishi na hiyo hali "
Kujifunza kuishi na tatizo badala ya kulitafutia ufumbuzi ni kama kusafiri baharini bila dira.
"Nini kifanyike"
¤Kukaa nae karibu na kumpatia msaada.
¤Hupaswi kumvunja moyo na kumkatisha tamaa kwa namna yoyote ile.
¤Ongea nae ili uweze kufahamu anacho fikiria kutenda hii itakufanya ujue kama anawaza kufanya maamuzi magumu na kuangalia namna ya kumsaidia .
Ni rafiki yako :Michael Angelo Togo
Barua pepe :michaeltogo99@gmail.com
0766746918 (whatsap)
0 maoni: